Kwa haraka haraka tuu ninachoweza kukuambia msomaji wangu ni kuwa kama haujafika Afrika Kusini ni kuwa kwa sie bongo tunawazidi kwa mpangilio mzuri wa uvaaji.
Ni kweli wao wana nguo nzuri na bidhaa nyingine za urembo ila kinachokosekana nadhani ni mpangilio.
Mfano nimeona wadada wengi hapa Johannesburg wakiwa na aina moja au mbili tuu za nywele yaani ni dread au ni rasta. Kimavazi ni kama wana mavazi ya aina ile ile karibu wote. Sina maana wanavaa nguo za aina moja, ila ni watu wa kuendana na mtindo sana hivyo mtindo au mitindo iliyo maarufu kwa wakati husika iwe ni nywele au mavazi basi ndio itakayotumiwa sana.
Wenzetu wamejaliwa malls kibao tena kubwa kubwa , yaani hata vitongoji vidogo tuu utakuta ina mall kubwa kuliko hata hiyo ya kwetu ya Mlimani City. Ukiingia sasa huko kwenye mall, maduka ni mengi na yana bidhaa nzuri kweli kweli.
Kwa binafsi nimevutiwa sana na viatu vyao na bidhaa za urembo kama vipodozi.
Mall hapa Johannesburg nilipofikia. |
Bado ni mapema kusema sana kuhusu urembo ndani ya Afrika ya Kusini, nitakapokamilisha kutembelea mji mwingine mkubwa wa Cape Town, nitakujuza zaidi.
Ila bila shaka ni sehemu ya kutembelea na kujifunza mengi.
Nikiwa na mwenyeji wangu tukielekea mjini. |
Nikisubiria kifungua kinywa hapa Edenvale, Johannesburg |
0 comments :
Post a Comment