Usafi wa uso ni
moja ya mambo muhimu sana kwa mwanamke au mwanaume yeyote yule ambaye
anapenda kuwa nadhifu na mwenye mvuto. Kumbuka “reception ndio kila kitu “.
Unapokutana na mtu sura yako na mwonekano wa sura yako ndio kitu cha kwanza
kinachomtambulisha kwamba wewe ni nani na upo kwenye hali gani.
Kuna njia nyingi za
kuufanya uso wako uvutie na kupendeza. Leo tutaongelea zaidi jinsi ya kusafisha
uso kwa njia ya asili. Mie hupenda
kutumia njia ya asili sababu ni rahisi kupata vifaa na ni nafuu . Pia mtu
anaweza kufanya kwa mazingira yoyote yale. Na matumizi ya vitu vya asili kwenye
mwili husaidia kupunguza sumu mwilini kwani kitumia vipodozi vyenye kemikali
husababisha miili yetu kujaaa sumu.
Njia ya asili ya
kusafisha na kupendezesha mwili ninayokueleza leo inahitaji vitu vikuu vinne :
asali, sukari, maziwa, na limao.
Haijalishi aina gani ya
ngozi unayo , njia hii ya asili inaweza kutumika kwa aina yoyote ile ya ngozi
iwe ngozi yenye mafuta au ngozi kavu.
Kiasi cha mahitaji
yanayohitajika:
- Kijiko kimoja cha asali
- Kijiko kimoja cha sukari
- Kijiko kimoja cha maziwa
- Kijiko kimoja cha limao
Utaratibu wa kusafisha
uso
Weka mahitaji hapo juu kwenye chombo kilicho kisafi,
changanya vitu vyako mpaka vilainike, viache kwa muda wa dk 10 ili viweze
kuchanganyikana vizuri na na sukari iweze kuyayuka vizuri.
Baada ya mchanganyiko
wako kuwa tayari chukua kipande cha pamba kilicho kisafi tumia kupakia
mchanganyiko wako usoni . Na kumbuka ni vizuri uso ukiwa mchafu na upaswi
kuosha uso alafu ufanye zoezi hili.Baada ya kupaka mchanganyiko wako
usoni kaa kwa dk 15 .
Baada ya hapo chukua
maji ya uvuguvugu, kitaulo kisafi na sabuni ya kipande “vizuri kutumia sabuni
ya kipande maana haina kemikali nyingi” tumia kitambaa kuoshea uso wako
pamoja na sabuni.
Basi baada ya hapo
umekuwa umemaliza zoezi lako la usafi wa ngozi yako
Kumbuka njia hii aina madhala yoyote na haibadilishi rangi au muonekano wa ngozi yako na unashauliwa kufanya mara kwa mara ili kukupa mvuto zaidi.
Just pray to Allah utaona unanawiri uso wako.
ReplyDeleteExactly Asilimia 100%
DeleteI will try this
ReplyDeleteNtajaribu
ReplyDelete