EPUKA NYWELE ZINAZOKATIKA KWA KUTUMIA KITUNGUU MAJI

Kitunguu maji kina sulphur ambayo husaidia kutengeneza  tishu za collagen katika mwili ambapo collagen husaidia kunurisha nywele na ngozi. Hivyo tunaweza kusema kuwa kitunguu maji husaidia kukuza nywele na kwa wale wenye nywele za kukatika, kupaka kitunguu maji mara kwa mara kinaweza kusaidia kupambana na tatizo hilo.

Je utatumiaje kitunguu ili ufaidike na kitunguu maji kwa nywele zako. Soma zaidi hapa chini.

Jinsi ya kuandaa
  • Chukua kitunguu kimoja au viwili kutegemeana na ukubwa wa kitunguu chenyewe. Fuata hatua zifuatazo:
  • Osha vizuri kitunguu au vitunguu na kisha ukimenye au uvimenye
  • Kata kitunguu au vitunguu vipande vidogo vidogo ili iwe rahisi kusaga au kutwanga
  • Saga kwenye brenda au twanga kwenye kinu , njia yoyote ile ambayo kwako ni rahisi kwako.  Visage au vitwange mpaka vilainike kabisa ili uweze  kutoa maji kwa urahisi.
  • Ukishasaga au kutangwa vitunguu , vichuje  vizuri ili upate maji maji .Zingatia usiweke maji kwa hivi vitunguu.

Jinsi ya kupaka
Nywele sio lazima ziwe safi maana  unapaswa  kuziosha  baada ya kupaka maji ya vitunguu.
  • Chukua pamba ambayo utatumia kupaka hayo maji ya vitunguu kwenye nywele zako. Paka zile sehemu ambazo nywele zimekatika. Unaweza pia paka  kichwa kizima.
  • Baada ya kupaka  unapaswa kuvaa kofia ya plastic na kitambaa kwa juu ili kuweza kupata joto . Tahadhali usikae kwenye mashine ya steam au dryer.
  • Ukiwa na kofia ya plastic na kitambaa kwa juu ya nywele zako , ukae hivyo hivyo kwa masaa  manne hadi matano.
  • Baada ya hapo unaweza kuosha na kukausha nywele zako na kuweka style yoyote ile.
Hitimisho
Ni vema kufanya zoezi hili la kupaka vitunguu walau mara mbili kwa mwezi. Ikiwa harufu ya kitunguu ni kali, unaweza weka asali kidogo kwenye maji ya vitunguu.
Kwa matokeo mazuri  ya kukuza na kutunza nywele zako tumia vitunguu vidogo kufanya zoezi nililoeleza hapo juu.

0 comments :

Post a Comment