Mapenzi ni furaha haswa pale unapompata mtu sahihi na kwa wakati sahihi. Hata hivyo kama ulishaumizwa katika mahusiano hapo kabla , inaweza kuwa ngumu sana kujua kama upo tayari kuingia katika uhusiano mwingine.
Wasiwasi, woga na kutokujua
kama upo tayari kwa mahusiano mapya kunaweza kutokana na uzoefu wako wa
mahusiano yako yaliyopita, au mapungufu yako mengine ambayo kupitia uhusiano
wako uliopita umegundua na hivyo kujiwekea wakati mgumu wa kujiamini na kutaka kuanza
mahusiano mapya
Kwa wadada kama mimi kuanza
mahusiano mapya kunaweza kuwa kugumu uwe na ujauzito na hatimaye kujifungua
mtoto, sasa unajiuliza kama huyo mpenzi mpya atakukubali wewe pamoja na mtoto
wako. Na sio tuu kukukubali wewe na mtoto au watoto, bali zaidi sana kukubali
historia yako na kwamba sasa umejifunza na unataka kuwa mtu bora Zaidi.
Ukitafakari na kuelewa kuwa
mapenzi ni zaidi ya hisia za mwili, kwamba mapenzi ni watu wawili wapendanao
wanaamua kujenga ushirika ili kwa pamoja waweze kufikia ndoto binafsi na pia
kujenga ndoto za pamoja na kuishi thamani haswa ya maisha ambayo ni kushare na
mtu mambo mengi, muda na hisia za kimapenzi, ukitafakari hivyo, unajikuta
unakaribia kufikia jibu la wakati gani ni sahihi kuanza mahusiano mapya.
Kwa upande wangu sioni jibu la
moja kwa muda kwamba wakati gani ni sahihi. Kwani wakati kuwa sahihi haitegemei
tuu wewe kama wewe, inategemea pia huyo utakayekua nae.
Nijuacho mie ni kuwa :
1.Kutoingia kwenye uhusiano
mpya eti kwa sababu unataka kumsahau huyo mpenzi wako aliyepita. Huo hautokua
wakati sahihi.
2.Kutoingia kwenye uhusiano
mpya eti kwakua unapata presha toka kwa wazazi, marafiki , au ndugu kuwa muda
umefika wa wewe kuwa na mpenzi au ndoa.
3.Kutoingia kwenye uhusiano
mpya eti kwakuwa unajisikia tuu mpweke, hivyo unahitaji “kampani”
4.Kutoingia kwenye uhusiano
mpya eti kwakuwa una matatizo ya kifedha, au unatafuta ajira , n.k
Kingine ni kuwa:
Tumia muda wa kutosha toka
uhusiano uliopita hadi uhusiano mpya. Usianze mahusiano mapya kwa ghafla. Tumia
muda wa kutosha kuwa peke yako, ukijihoji na kutafakari nini haswa unataka
katika uhusiano mpya. Jifunze kutoka katika mahusiano yako yaliyopita, jifunze
toka katika mahusiano ya watu wengine.
Endelea kufanya mawasiliano na
watu wa jinsia nyingine ukichunguza kwa makini katika mazungumzo na mwonekano
wa watu hao wa jinsia tofauti ni yupi anaweza haswa kuwa mpenzi wako mpya.
Penda kujua zaidi kuhusu yule utakayemuona ana muelekeo wa aina ya mwanaume au
mwanamke unayemtaka.
Fanya urafiki wa muda mrefu,
hapa namaanisha msiwe wapenzi. Muwe kwanza marafiki na huyo utakayekuwa
umemchunguza na kumuona ana sifa unazotaka. Hata hivyo usijekata tamaa, kuna
mambo mengi huwezi jifunza toka kwa rafiki mpaka muwe wapenzi.
Sasa zamu yako wewe msomaji,
je wewe unafikiri ni muda gani muafaka wa kuanza mahusiano mapya ?
nice blog, nimeipenda, mm ndo niliye kukuta jana stationary, unaweza cheki yangu inaitwa WISEMIC BLOG ambayo unaweza ipata hapa wisemic.blogspot.com
ReplyDelete