Kwa haraka haraka tuu ninachoweza kukuambia  msomaji wangu ni kuwa kama haujafika Afrika Kusini ni kuwa kwa sie bongo tunawazidi kwa mpangilio mzuri wa uvaaji.
Ni kweli wao wana nguo nzuri na bidhaa nyingine za urembo ila kinachokosekana nadhani ni mpangilio.

Mfano nimeona wadada wengi hapa Johannesburg wakiwa na aina moja au mbili tuu za nywele yaani ni dread au ni rasta. Kimavazi ni kama wana mavazi ya aina ile ile karibu wote. Sina maana wanavaa nguo za aina moja, ila ni watu wa kuendana na mtindo sana hivyo mtindo au mitindo iliyo maarufu kwa wakati husika iwe ni nywele au mavazi basi ndio itakayotumiwa sana.



Wenzetu wamejaliwa malls kibao tena kubwa kubwa , yaani hata vitongoji vidogo tuu utakuta ina mall kubwa kuliko hata hiyo ya  kwetu ya Mlimani City. Ukiingia sasa huko kwenye mall, maduka ni mengi na yana bidhaa nzuri kweli kweli. 
Kwa binafsi nimevutiwa sana na viatu vyao na bidhaa za urembo kama vipodozi.
Mall hapa Johannesburg nilipofikia.

Bado ni mapema kusema sana kuhusu urembo ndani ya Afrika ya Kusini, nitakapokamilisha kutembelea mji mwingine mkubwa wa Cape Town, nitakujuza zaidi.

Ila bila shaka ni sehemu ya kutembelea na kujifunza mengi.
Nikiwa na mwenyeji wangu tukielekea mjini.
Nikisubiria kifungua kinywa hapa Edenvale, Johannesburg


Kitunguu maji kina sulphur ambayo husaidia kutengeneza  tishu za collagen katika mwili ambapo collagen husaidia kunurisha nywele na ngozi. Hivyo tunaweza kusema kuwa kitunguu maji husaidia kukuza nywele na kwa wale wenye nywele za kukatika, kupaka kitunguu maji mara kwa mara kinaweza kusaidia kupambana na tatizo hilo.

Je utatumiaje kitunguu ili ufaidike na kitunguu maji kwa nywele zako. Soma zaidi hapa chini.

Jinsi ya kuandaa
  • Chukua kitunguu kimoja au viwili kutegemeana na ukubwa wa kitunguu chenyewe. Fuata hatua zifuatazo:
  • Osha vizuri kitunguu au vitunguu na kisha ukimenye au uvimenye
  • Kata kitunguu au vitunguu vipande vidogo vidogo ili iwe rahisi kusaga au kutwanga
  • Saga kwenye brenda au twanga kwenye kinu , njia yoyote ile ambayo kwako ni rahisi kwako.  Visage au vitwange mpaka vilainike kabisa ili uweze  kutoa maji kwa urahisi.
  • Ukishasaga au kutangwa vitunguu , vichuje  vizuri ili upate maji maji .Zingatia usiweke maji kwa hivi vitunguu.

Jinsi ya kupaka
Nywele sio lazima ziwe safi maana  unapaswa  kuziosha  baada ya kupaka maji ya vitunguu.
  • Chukua pamba ambayo utatumia kupaka hayo maji ya vitunguu kwenye nywele zako. Paka zile sehemu ambazo nywele zimekatika. Unaweza pia paka  kichwa kizima.
  • Baada ya kupaka  unapaswa kuvaa kofia ya plastic na kitambaa kwa juu ili kuweza kupata joto . Tahadhali usikae kwenye mashine ya steam au dryer.
  • Ukiwa na kofia ya plastic na kitambaa kwa juu ya nywele zako , ukae hivyo hivyo kwa masaa  manne hadi matano.
  • Baada ya hapo unaweza kuosha na kukausha nywele zako na kuweka style yoyote ile.
Hitimisho
Ni vema kufanya zoezi hili la kupaka vitunguu walau mara mbili kwa mwezi. Ikiwa harufu ya kitunguu ni kali, unaweza weka asali kidogo kwenye maji ya vitunguu.
Kwa matokeo mazuri  ya kukuza na kutunza nywele zako tumia vitunguu vidogo kufanya zoezi nililoeleza hapo juu.


Usafi wa  uso ni moja ya mambo muhimu sana kwa mwanamke au mwanaume yeyote  yule ambaye anapenda kuwa nadhifu na mwenye mvuto. Kumbuka “reception  ndio kila kitu “. Unapokutana na mtu sura yako na mwonekano wa sura yako ndio kitu cha kwanza kinachomtambulisha kwamba wewe ni nani  na upo kwenye hali gani.

Kuna njia nyingi za kuufanya uso wako uvutie na kupendeza. Leo tutaongelea zaidi jinsi ya kusafisha uso kwa njia ya asili.  Mie hupenda kutumia njia ya asili sababu ni rahisi kupata vifaa na ni nafuu . Pia mtu anaweza kufanya kwa mazingira yoyote yale. Na matumizi ya vitu vya asili kwenye mwili husaidia kupunguza sumu mwilini kwani kitumia vipodozi vyenye kemikali husababisha miili yetu kujaaa sumu.

Njia ya asili ya kusafisha na kupendezesha mwili ninayokueleza leo inahitaji vitu vikuu vinne : asali, sukari, maziwa, na limao.

Haijalishi aina gani ya ngozi unayo , njia hii ya asili inaweza kutumika kwa aina yoyote ile ya ngozi iwe ngozi yenye mafuta au ngozi kavu.

Kiasi cha mahitaji yanayohitajika:

  • Kijiko kimoja cha asali
  • Kijiko kimoja cha sukari
  • Kijiko kimoja cha maziwa
  • Kijiko kimoja cha limao


Utaratibu wa kusafisha uso
Weka  mahitaji hapo juu kwenye chombo kilicho kisafi, changanya vitu vyako mpaka vilainike, viache kwa muda wa dk 10 ili viweze kuchanganyikana vizuri na  na sukari iweze kuyayuka vizuri.
Baada ya mchanganyiko wako kuwa tayari  chukua kipande cha pamba kilicho kisafi tumia kupakia mchanganyiko wako usoni . Na kumbuka ni vizuri uso ukiwa mchafu  na upaswi kuosha uso alafu ufanye  zoezi hili.Baada ya kupaka mchanganyiko wako usoni  kaa kwa dk 15 .
Baada ya hapo chukua maji ya uvuguvugu, kitaulo kisafi na sabuni ya kipande “vizuri kutumia sabuni ya kipande maana haina kemikali nyingi” tumia kitambaa  kuoshea uso wako pamoja na sabuni.
Basi baada ya hapo umekuwa umemaliza zoezi lako la usafi wa ngozi yako

Kumbuka njia hii aina madhala yoyote na haibadilishi rangi au muonekano wa ngozi yako na unashauliwa kufanya mara kwa mara  ili kukupa mvuto zaidi.
Ukiwa na mwili unaoupenda kunakufanya ujiamini na uwe na furaha, na hivyo kujifungulia fursa nyingi katika maisha yako. Kuna msemo unasema :” When you look good, you feel good, and when you feel good, you do good” Yaani kama ukionekana vizuri, utajisikia vizuri, ukijisikia vizuri, utafanya mambo mazuri.
Hivyo inapofikia hatua mtu hufurahii uzito na ukubwa wa mwili wako, bila shaka unahitaji kuchukua hatua ya ziada ili kuudhibiti huo mwili na kuurudisha katika muonekano unaoutaka wewe. Kama upo katika hali hiyo basi usikate tamaa na kujichukia. Bado unayo nafasi ya kuutengeneza mwili wako vile utakavyo.
Leo nikueleze mbinu 10 ambazo watu wengi wamezitumia na zimeonyesha mafanikio makubwa katika kupunguza mwili. Njia hizi ni salama na za haraka kama ukifuata kwa uhakika kama inavyoshauriwa.
Kupungua mwili kunaaanza kwa jinsi vile ulivyo  weka kipaumbele wa swala zima. Unahitaji kupanga muda haswa na kujituma ili ufikie kuutengeneza mwili wako vile utakavyo.
Muhimu kuzingatia:
Kabla haujanza mpango huu wa kupunguza uzito unapaswa kujua una kilo ngapi na lengo lako unapaswa kuwa na kilo ngapi na baada ya   muda gani.
Kupanga muda sahihi kunakusaidia kuweka malengo  ya kwamba ndani ya kipindi gani au muda gani unataka  uwe umepunguza kilo ngapi. Kwa mfano unaweza weka  kwamba ndani ya mwezi mmoja uwe umepungua kilo 10.Kwenye mwezi mmoja unaweza weka malengo kila wiki unapungua kilo 3 .
Ninaposema kilo 3 maana yake unaweza kutimiza hicho kiwango au kupunguza zaidi ukawa chini ya kiwango.
Mbinu sahihi za kufuata ili kuweza kupunguza uzito.
1) Tambua mahitaji ya Calories (karolis) kwenye mwili wako:    Carolies ni neno la kitaalam linalomanisha kiasi cha nguvu (energy) inayoingia au unayoitoa kuitoa katika mwili wako. Watu tofauti tofauti huwa na mahitaji tofauti ya calories. Fanya mpango umuone mtaalamu wa lishe akusaidie ujue kiwango halisi cha calories unachohitaji kuingiza kwa siku na kiasi gani unatakiwa kutoa kwa siku.
Kutoa au kupunguza calories unatakiwa ufanye mazoezi madogo madogo na pia uwe makini na calories unazoingiza.
 2) Matumizi ya matunda na mboga za majani kwa wingi zaidi.
3)Punguza kiwango cha  chakula  .kupunguza kiwango cha chakula maana yake kama ulikuwa unakula sahani 2 kwa mlo au chakula kilichokingi basi punguza sana sana sahani moja tuu.
4)Tumia nyama nyeupe kwa wingi na zilizoiva vizuri zaidi.
5)Usithibiti sana vyakula unaweza kula vyakula uvipendavyo lakini kwa kiwango kidogo sana.kama nyama ,chips, chocolate
6)Epuka sana matumiz ya soda , bia na juice za viwandani.badala yake tumia juice za asili ukiepuka sukari.
7)Maji yafanye kuwa sehemu ya maisha yako  na unywaji mwingi wa maji kuna kusaidia kutokuwa na njaa za mara kwa mara. Na unashauriwa  kunywa maji nusu saa kabla ya kula na baada ya kula.
8) Epuka kula chakula na kwenda kulala au kukaa sehemu moja. Baada ya kula chakula unashauriwa   kufanya kazi kidogo ili chakula kiweze kupungua.
9) Kwa wale wenye magari punguza  matumizi ya gari zaidi tumia mda mwengine kutembea umbali mfupi . Asilimia kubwa ya watu wa mjini wanakuwa wanene kwa matumizi ya magari na  bodaboda na bajaji mwili unakuwa haupati zoezi au kuchangamka.Jitahidi kutembea umbali mfupi kwa Afya zaidi.
10) Kuwa na heshima  na mwili wako na kuwa makini na kila ambacho unaingiza kwenye mwili wako . Punguza msongo wa mawazo kwani inaweza athiri tabia yako ya ulaji , ukajikuta unakula sana na bila mpangilio.

Kutaka kupunguza mwili kuna kuja na nidhamu ya yako ya kuheshimu matakwa ya mwili wako kuwa bora  na kutoka hatua moja kwenda nyingine.

Mapenzi ni furaha haswa pale unapompata mtu sahihi na kwa wakati sahihi.  Hata hivyo kama ulishaumizwa katika mahusiano hapo kabla , inaweza kuwa ngumu sana kujua kama upo tayari kuingia katika uhusiano mwingine.

Wasiwasi, woga na kutokujua kama upo tayari kwa mahusiano mapya kunaweza kutokana na uzoefu wako wa mahusiano yako yaliyopita, au mapungufu yako mengine ambayo kupitia uhusiano wako uliopita umegundua na hivyo kujiwekea wakati mgumu wa kujiamini na kutaka kuanza mahusiano mapya
Kwa wadada kama mimi kuanza mahusiano mapya kunaweza kuwa kugumu uwe na ujauzito na hatimaye kujifungua mtoto, sasa unajiuliza kama huyo mpenzi mpya atakukubali wewe pamoja na mtoto wako. Na sio tuu kukukubali wewe na mtoto au watoto, bali zaidi sana kukubali historia yako na kwamba sasa umejifunza na unataka kuwa mtu bora Zaidi.
Ukitafakari na kuelewa kuwa mapenzi ni zaidi ya hisia za mwili, kwamba mapenzi ni watu wawili wapendanao wanaamua kujenga ushirika ili kwa pamoja waweze kufikia ndoto binafsi na pia kujenga ndoto za pamoja na kuishi thamani haswa ya maisha ambayo ni kushare na mtu mambo mengi, muda na hisia za kimapenzi, ukitafakari hivyo, unajikuta unakaribia kufikia jibu la wakati gani ni sahihi kuanza mahusiano mapya.
Kwa upande wangu sioni jibu la moja kwa muda kwamba wakati gani ni sahihi. Kwani wakati kuwa sahihi haitegemei tuu wewe kama wewe, inategemea pia huyo utakayekua nae.
Nijuacho mie ni kuwa :
1.Kutoingia kwenye uhusiano mpya eti kwa sababu unataka kumsahau huyo mpenzi wako aliyepita. Huo hautokua wakati sahihi.
2.Kutoingia kwenye uhusiano mpya eti kwakua unapata presha toka kwa wazazi, marafiki , au ndugu kuwa muda umefika wa wewe kuwa na mpenzi au ndoa.
3.Kutoingia kwenye uhusiano mpya eti kwakuwa unajisikia tuu mpweke, hivyo unahitaji “kampani”
4.Kutoingia kwenye uhusiano mpya eti kwakuwa una matatizo ya kifedha, au unatafuta ajira , n.k
Kingine ni kuwa:
Tumia muda wa kutosha toka uhusiano uliopita hadi uhusiano mpya. Usianze mahusiano mapya kwa ghafla. Tumia muda wa kutosha kuwa peke yako, ukijihoji na kutafakari nini haswa unataka katika uhusiano mpya. Jifunze kutoka katika mahusiano yako yaliyopita, jifunze toka katika mahusiano ya watu wengine.

Endelea kufanya mawasiliano na watu wa jinsia nyingine ukichunguza kwa makini katika mazungumzo na mwonekano wa watu hao wa jinsia tofauti ni yupi anaweza haswa kuwa mpenzi wako mpya. Penda kujua zaidi kuhusu yule utakayemuona ana muelekeo wa aina ya mwanaume au mwanamke unayemtaka.
Fanya urafiki wa muda mrefu, hapa namaanisha msiwe wapenzi. Muwe kwanza marafiki na huyo utakayekuwa umemchunguza na kumuona ana sifa unazotaka. Hata hivyo usijekata tamaa, kuna mambo mengi huwezi jifunza toka kwa rafiki mpaka muwe wapenzi.

Sasa zamu yako wewe msomaji, je wewe unafikiri ni muda gani muafaka wa kuanza mahusiano mapya ?